Swali: Mtunzi amenyofoa dondoo kuhusu kwambaa Sutrah ya swalah ni lazima iwe safi.

Jibu: Kutokana na Hadiyth ya Asmaa´ alipomwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”… ioshe kisha uswali ndani yake.”

Ni dalili kwamba haifai kuswali nayo ikiwa iko na najisi. Ni lazima pia kinachokufunika kiwe kisafi na mwili mzima. Ni lazima vitu vitatu viwe visafi:

1 – Mwili.

2 – Maeneo ya kuswalia.

3 – Mavazi ambayo mtu anaswali nayo.

Ni lazima vyote hivo viwe visafi. Maneno Yake (Jalla wa ´Alaa):

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ

“Na nguo zako zitwaharishe!”[1]

Yanakusanya vyote viwili.

Swali: Lakini Sutra si maeneo wala mavazi?

Jibu: Kinachokufunika ambacho unakivaa, na si Sutrah unayoiweka mbele yako. Anachokusudia ni mavazi. Hivo ndivo anavokusudia. Ni kile kinachomfunika mwanamke huyo. Ama Sutrah inayowekwa mbele ya mswaliji si sharti iwe safi. Kinachozingatiwa ni mavazi yanayostiri mwili wa mwanamke huyo ambayo lazima yawe safi, ni mamoja kwa mwanamume na mwanamke.

[1] 74:04

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24689/هل-طهارة-السترة-شرط-لصحة-لصلاة
  • Imechapishwa: 26/11/2024