Uoshaji wa sehemu za siri wakati wa kutawadha

Swali: Je, nywele za sehemu za siri ni miongoni mwa viungo vya wudhuu´?

Jibu: Nywele za sehemu za siri si miongoni mwa viungo vya wudhuu´ wala si miongoni mwa sehemu zinazohusiana na kutamba kwa maji. Hata hivyo ikiwa najisi itazifikia wakati wa kujisaidia, basi ni wajibu kuosha sehemu iliyofikiwa na najisi.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/237)
  • Imechapishwa: 06/11/2026