Swali: Ninaumia kati ya vidole vya miguu kwa sababu ya maji wakati wa wudhuu´, kiasi kwamba sehemu iliyo kati ya vidole huwashwa sana na kujeruhiwa. Lakini maji yakikoma kuwafikia, baada ya siku maumivu na muwasho hupungua. Naomba mniongoze: kabla ya kutawadha, je, inajuzu kwangu kutawadha bila kuosha miguu au nipanguse juu ya soksi?
Jibu: Ikiwa hali ni kama ulivyoeleza, vaa soksi ukiwa katika twahara kamili, kisha katika kila wudhuu´ pangusa juu ya soksi hizo kwa muda wa mchana mmoja na usiku wake ukiwa mkazi, na michana mitatu pamoja na nyusiku zake ukiwa msafiri, muda wa kuwa hujapatwa na janaba. Ama ukipatwa na janaba basi ni wajibu kwako kuosha mwili wako wote, pamoja na miguu.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/245)
- Imechapishwa: 06/11/2026
Swali: Ninaumia kati ya vidole vya miguu kwa sababu ya maji wakati wa wudhuu´, kiasi kwamba sehemu iliyo kati ya vidole huwashwa sana na kujeruhiwa. Lakini maji yakikoma kuwafikia, baada ya siku maumivu na muwasho hupungua. Naomba mniongoze: kabla ya kutawadha, je, inajuzu kwangu kutawadha bila kuosha miguu au nipanguse juu ya soksi?
Jibu: Ikiwa hali ni kama ulivyoeleza, vaa soksi ukiwa katika twahara kamili, kisha katika kila wudhuu´ pangusa juu ya soksi hizo kwa muda wa mchana mmoja na usiku wake ukiwa mkazi, na michana mitatu pamoja na nyusiku zake ukiwa msafiri, muda wa kuwa hujapatwa na janaba. Ama ukipatwa na janaba basi ni wajibu kwako kuosha mwili wako wote, pamoja na miguu.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/245)
Imechapishwa: 06/11/2026
https://firqatunnajia.com/anaumia-na-kuwashwa-sana-anapoosha-miguu-yake-wakati-wa-kutawadha/