Uniaba na ujitoleaji katika ´Aqiyqah

Swali: Kuna mtu aliweka nadhiri kwa ajili ya Allaah kwamba Allaah akimjaalia rafiki yake mtoto basi atamfanyia ´Aqiyqah ambapo Allaah akamjaalia mtoto. Akitekeleza nadhiri yake baba yake hana haja tena ya kumfanyia ´Aqiyqah?

Jibu: Ndio. Inafaa kufanya uniaba. Akisimamia mtu mwengine kwa niaba yako au akajitolea kutoka katika pesa zake ni sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (42)
  • Imechapishwa: 28/06/2024