Unayotakiwa kusema wakati wa kuchinja Udhhiyah

Wakati wa kuchinja atasema:

باسم الله والله أكبر

“Kwa jina la Allaah na Allaah ni mkubwa.”

Haya ndio yamewekwa katika Shari´ah.

Akisema:

باسم الله

“Kwa jina Allaah.”

pekee, inasihi. Hata hivyo bora ni yeye kusema:

باسم الله والله أكبر

“Kwa jina la Allaah na Allaah ni mkubwa.”

Akiongeza kwa kusema:

إن صلاتي ونسكي ومحياي ومماتي لله رب العالمين، لا شريك له وبذلك أمرت وأنا من المسلمين

“Hakika swalah yangu na kichinjwa changu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu, hali ya kuwa hana mshirika; na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni katika waislamu.”

au akasema:

وَجَّهْتُ وَجْهِي للَّذِي فَطرَ السَّمَواتِ والأَرْضَ حَنيفاً وَما أَنا مِنَ الْمُشْرِكِينَ

“Nimeuelekeza uso wangu kwa yule ambaye Ameumba mbingu na ardhi, hali ya kumtakasia Yeye dini yangu na sikuwa mimi ni katika washirikina.”,

inapendeza. Hata hivyo inatosha akisema:

باسم الله والله أكبر

“Kwa jina la Allaah na Allaah ni mkubwa.”

Inatosha kusema hivo. Hivo ndivo alivokuwa akifanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakati mwingine pengine akazidisha:

إن صلاتي ونسكي ومحياي ومماتي لله رب العالمين، لا شريك له وبذلك أمرت وأنا من المسلمين

“Hakika swalah yangu na kichinjwa changu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah pekee, Mola wa walimwengu, hali ya kuwa hana mshirika; na kwa hayo ndio nimeamrishwa, nami ni katika waislamu.”

Wajibu ni kusema:

باسم الله

“Kwa jina la Allaah.”

Hivo ndio wajibu. Nyongeza:

والله أكبر

“Na Allaah ni mkubwa.”,

inapendeza.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/17196/حكم-الاضحية-في-عيد-الاضحى-وكيفيتها
  • Imechapishwa: 13/06/2024