´Abdullaah bin az-Zubayr (Radhiya Allaahu ´anh) alipokuwa akisikia radi huacha kusema na husema:

سُبْحَانَ الذي يُسَبِّحُ الرَّعْدُ بِحَمْدِهِ والْملائِكَةُ مِنْ خِيفَتِهِ

“Ametakasika yule ambaye radi zinamtakasa kwa himdi Zake na Malaika pia kwa kumuogopa.”[1]

Ka´b amesema:

“Yeyote atakayesema hivi mara tatu basi atasalimsihwa na radi hiyo.”

at-Tirmidhiy amepokea kwamba ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alipokuwa anasikia sauti ya radi na radi husema:

اللهم لا تقتلنا بغضبك، ولا تهلكنا بعذابك، وعافنا قبل ذلك

“Ee Allaah! Usituue kwa ghadhabu Yako, usituangamize kwa adhabu Yako. Tusamehe kabla ya hapo!”[2]

[1] Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib” (129).

[2] at-Tirmidhiy (3450), aliyesema kuwa Hadiyth ni ngeni, na Ahmad (2/457). Swahiyh kwa mujibu wa al-Haakim (4/286), ambayo imenyamaziwa na adh-Dhahabiy. Nzuri kwa mujibu wa al-´Iraaqiy katika “al-Mughniy ´an Haml-il-Asfaar” (1/295). Dhaifu kwa mujibu wa an-Nawawiy katika “al-Adhkaar” (1/471) na al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (3450).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 318-319
  • Imechapishwa: 22/09/2025