Miongoni mwa wasia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh) alimpomtuma kwa Ahl-ul-Kitaab Yemen:
“… chukua [mali] kutoka kwa matajiri wao na uwape mafukara wao.”
Hii ni dalili yenye kuonyesha lau mtawala atachukua zakaah kutoka kwa matajiri na kuwapa wale wenye kuistahiki basi mtoaji atakuwa ametekeleza dhimmah yake. Lakini lau mtu atasema kuwa haamini mtu aichukue naakaja kuichezea kwa kuitumia kinyume na njia inayotakikana. Jibu ni kwamba wewe ukitekeleza lile ambalo ni wajibu kwako basi utakuwa umetekeleza dhimmah yako, ni mamoja ikiwa itatumiwa kwa njia sahihi au kinyume.
Lakini Imaam Ahmad amesema kuwa lau mtu ataona kuwa kiongozi haitumii kwa kuwapa wale wenye kuistahiki, basi asimpe nayo isipokuwa ikiwa kama atamuomba nayo na kumlazimisha. Katika hali hiyo hapo atakuwa ametekeleza dhimmah yake.
Kujengea juu ya hili ni sawa kwa mtu akaficha kitu katika mali yake ikiwa yule anayempa haitumii kuwapa wale wenye kuistahiki. Atafanya hivo ili yeye mwenyewe aweze kujitolea zakaah ambayo ni wajibu kwake.
Lau tutakadiria kuwa mtawala atachukua kiwango zaidi ya kile ambacho ni wajibu, hiyo ni dhuluma na si halali kwa mtawala. Ama kuhusu mmiliki wa mali, ni juu yake kusikiliza na kutii. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Sikiliza na utii hata kama atakupiga mgongo wako na kuchukua mali yako.”
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/506-507)
- Imechapishwa: 23/09/2025
Miongoni mwa wasia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh) alimpomtuma kwa Ahl-ul-Kitaab Yemen:
“… chukua [mali] kutoka kwa matajiri wao na uwape mafukara wao.”
Hii ni dalili yenye kuonyesha lau mtawala atachukua zakaah kutoka kwa matajiri na kuwapa wale wenye kuistahiki basi mtoaji atakuwa ametekeleza dhimmah yake. Lakini lau mtu atasema kuwa haamini mtu aichukue naakaja kuichezea kwa kuitumia kinyume na njia inayotakikana. Jibu ni kwamba wewe ukitekeleza lile ambalo ni wajibu kwako basi utakuwa umetekeleza dhimmah yako, ni mamoja ikiwa itatumiwa kwa njia sahihi au kinyume.
Lakini Imaam Ahmad amesema kuwa lau mtu ataona kuwa kiongozi haitumii kwa kuwapa wale wenye kuistahiki, basi asimpe nayo isipokuwa ikiwa kama atamuomba nayo na kumlazimisha. Katika hali hiyo hapo atakuwa ametekeleza dhimmah yake.
Kujengea juu ya hili ni sawa kwa mtu akaficha kitu katika mali yake ikiwa yule anayempa haitumii kuwapa wale wenye kuistahiki. Atafanya hivo ili yeye mwenyewe aweze kujitolea zakaah ambayo ni wajibu kwake.
Lau tutakadiria kuwa mtawala atachukua kiwango zaidi ya kile ambacho ni wajibu, hiyo ni dhuluma na si halali kwa mtawala. Ama kuhusu mmiliki wa mali, ni juu yake kusikiliza na kutii. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Sikiliza na utii hata kama atakupiga mgongo wako na kuchukua mali yako.”
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/506-507)
Imechapishwa: 23/09/2025
https://firqatunnajia.com/unapoona-kuwa-mtawala-haitumii-mali-yako-ya-zakaah-kuwapa-wastahiki/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket