Unapokaa juu ya kipando cha mnyama mkorofi

Yuunus bin ´Ubayd amesema:

”Hakuna mtu yeyote ambaye amempanda mnyama mkorofi, akasema sikioni mwake:

أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ

”Je, wanataka dini isiyo ya Allaah na hali amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi kwa kupenda na kwa kutopenda na Kwake watarejeshwa?”[1]

isipokuwa atasimama kwa idhini ya Allaah  (Ta´ala).”

Shaykh wetu  (Rahimahu Allaah) amesema:

”Nilisema hivo na mambo yakawa namna hiyo.”[2]

[1] 3:83

[2] al-Kalim at-Twayyib, uk. 147. al-Albaaniy amesema:

“Ni yenye kukatika kwa sababu ni maneno ya Yuunus bin ´Ubayd. Hata kama ni mwanafunzi wa Maswahabah anayeaminika, cheni ya wapokezi hadi kwake si Swahiyh, kwa sababu ndani yake yumo al-Minhaal bin ´Iysaa, ambaye hatambuliki. Isitoshe jengine ni kwamba masimulizi yenye kukatika si hoja. Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema kuwa amejaribu jambo hilo, kama alivyotamka hayo wazi Ibn-ul-Qayyim katika “al-Waabil as-Swayyib”. Hata hivyo mambo ya Shari´ah hayathibitishwi kwa kujaribu.” (al-Kalim at-Twayyib, uk. 146-147)

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 334
  • Imechapishwa: 17/09/2025