Muslim amepokea ya kwamba Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Anapoingia mwanamume nyumbani kwake na akamtaja Allaah (Ta´ala) wakati wa kuingia na wakati wa chakula chake, basi shaytwaan husema: ”Hamna malazi kwenu wala chakula cha jioni.” Na akiingia pasi na kumtaja Allaah (Ta´ala) wakati wa kuingia kwake, shaytwaan husema: ”Mmekipata malazi.” Na asipotaja Allaah (Ta´ala) wakati wa chakula chake, husema: ”Mmekipata malazi na chakula cha jioni.”[1]
Abu Daawuud amepokea kutoka kwa Abu Maalik al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Anapoingia mtu nyumbani kwake, basi aseme:
اللهم إني أسألك خير المولج وخير المخرج، بسم الله ولجنا، وبسم الله خرجنا، وعلى الله ربنا توكلنا
“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba maingio mema na matokeo mazuri. Tunaingia ndani kwa jina la Allaah, tunatoka kwa jina la Allaah na tunamtegemea Allaah, Mola wetu.”
Kisha awasalimie watu wa nyumbani mwake.”[2]
at-Tirmidhiy amepokea ya kwamba Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliniambia: “Ewe mwanangu kipenzi! Unapowaingia kwa watu wa nyumbani mwako, basi watolee salamu. Itakuwa ni baraka juu yako na juu ya watu wa nyumbani mwako.”[3]
at-Tirmidhiy amesema:
”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”
[1] Muslim (2018).
[2] Abu Daawuud (5096). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (5096).
[3] at-Tirmidhiy (2698).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 262-263
- Imechapishwa: 23/09/2025
Muslim amepokea ya kwamba Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Anapoingia mwanamume nyumbani kwake na akamtaja Allaah (Ta´ala) wakati wa kuingia na wakati wa chakula chake, basi shaytwaan husema: ”Hamna malazi kwenu wala chakula cha jioni.” Na akiingia pasi na kumtaja Allaah (Ta´ala) wakati wa kuingia kwake, shaytwaan husema: ”Mmekipata malazi.” Na asipotaja Allaah (Ta´ala) wakati wa chakula chake, husema: ”Mmekipata malazi na chakula cha jioni.”[1]
Abu Daawuud amepokea kutoka kwa Abu Maalik al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh), ambaye amesimulia ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Anapoingia mtu nyumbani kwake, basi aseme:
اللهم إني أسألك خير المولج وخير المخرج، بسم الله ولجنا، وبسم الله خرجنا، وعلى الله ربنا توكلنا
“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba maingio mema na matokeo mazuri. Tunaingia ndani kwa jina la Allaah, tunatoka kwa jina la Allaah na tunamtegemea Allaah, Mola wetu.”
Kisha awasalimie watu wa nyumbani mwake.”[2]
at-Tirmidhiy amepokea ya kwamba Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliniambia: “Ewe mwanangu kipenzi! Unapowaingia kwa watu wa nyumbani mwako, basi watolee salamu. Itakuwa ni baraka juu yako na juu ya watu wa nyumbani mwako.”[3]
at-Tirmidhiy amesema:
”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”
[1] Muslim (2018).
[2] Abu Daawuud (5096). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (5096).
[3] at-Tirmidhiy (2698).
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 262-263
Imechapishwa: 23/09/2025
https://firqatunnajia.com/unapoingia-nyumbani/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket