Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ ۗ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّـهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ
“Bila shaka Tutakujaribuni kwa kitu katika khofu na njaa na upungufu wa mali na nafsi na mazao [katika kazi zenu]. Wabashirie wale wenye kusubiri ambao unapowafika msiba basi husema: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea – hao zitakuwa juu yao baraka kutoka kwa Mola wao na rehema na hao ndio wenye kuongoka.”[1]
Inasemekana kwamba Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:
”Mseme ´Hakika sisi ni wa Allaah na hakika Kwake ndio tutarejea` katika kila kitu hata inapohusiana na kamba ya viatu chake; kwani huo ni msiba.”[2]
Umm Salamah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Hakuna muislamu yeyote anayepatwa na msiba na akasema:
إِنَّا لله وإِنَّا إِلَيْه راجعونَ اللهُمَّ أَجِرْني في مُصِيبَتي وَأَخْلِفْ لي خَيْراً منها
”Hakika sisi ni wa Allaah na Kwake ndiko tutarejea. Ee Allaah! Nilipe kwa msiba wangu na Unipe badala yake kheri kuliko hiyo.”
isipokuwa humlipa kwa msiba wake na humpa badala ilio bora kuliko hiyo.”
Akasema:
”Wakati Abu Salamah alipofariki, nikasema kama alivyoamuru Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo Allaah akanipa mbora kuliko yeye; Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[3]
Amesema tena (Radhiya Allaahu ´anhaa):
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia kwa Abu Salamah ilihali macho yake yamemtoka ambapo akamfumba kisha akasema: “Roho inapochukuliwa inasindikizwa na macho.” Watu wakapiga makelele katika watu wake. Akasema: “Msijiombe dhidi ya nafsi zenu isipokuwa kwa kheri. Kwani Malaika huitikia “Aamiyn” kwa yale mnayoyasema.” Kisha akasema:
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِأَبِي سَلَمَةَ وَارْفَعْ دَرَجَتَهُ فِي الْمَهْدِيِّينَ، وَاخْلُفْهُ فِي عَقِبِهِ فِي الْغَابِرِينَ، وَاغْفِرْ لَنَا وَلَهُ يَا رَبَّ الْعَالَمِينَ، وَافْسَحْ لَهُ فِي قَبْرِهِ، وَنَوِّرُ لَهُ فِيهِ
“Ee Allaah! Msamehe Abu Salamah, ipandishe daraja yake katika wale waliotangulia, mkaimu kwa kizazi chake katika wale aliowaacha, msamehe yeye na sisi, ee Mola wa walimwengu, mpanulie ndani ya kaburi lake na umtilie nuru ndani yake.”[4]
[1] 2:155-157
[2] Dhaifu sana kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “al-Kalim at-Twayyib”, uk. 127.
[3] Muslim (918).
[4] Muslim (920).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 307-308
- Imechapishwa: 09/09/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 307-308
Imechapishwa: 09/09/2025
https://firqatunnajia.com/unapofikwa-na-msiba/