´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa akiona mwezi mwandamo husema:

الله أَكبر اللهُمَّ أَهِلَّهُ عَلَيْنَا بالأَمْنِ وَالإِيمانِ والسَّلاَمةِ والإِسْلاَمِ والتَّوْفيقِ لِمَا تُحِبُّ وَتَرْضى رَبُّنَا وَرَبُّكَ الله

“Allaah ni Mkubwa! Ee Allaah! Idhihirishe kwetu kwa amani, imani, usalama, Uislamu na tawfiyq ya kile unachokipenda na kukiridhia. Mola Wetu na Mola Wako ni Allaah!”[1]

Qataadah ameeleza kuwa amefikiwa na khabari kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema wakati alipoona mwezi mwandamo:

هِلَالُ خَيْرٍ وَرُشْدٍ، هِلَالُ خَيْرٍ وَرُشْدٍ، هِلَالُ خَيْرٍ وَرُشْدٍ، آمَنْتُ بِالَّذِي خَلَقَكَ

“Mwezi mwandamo wa kheri na uongofu. Mwezi mwandamo wa kheri na uongofu. Mwezi mwandamo wa kheri na uongofu. Nimemwamini Allaah ambaye amekuumba.”

Akisema hivo mara tatu halafu anasema:

الحَمْدُ للهِ الَّذِي ذَهَبَ بِشَهْرِ كَذَا، وَجَاءَ بِشَهْرِ كَذَا

”Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye amefanya kumalizika mwezi fulani na akaufanya kuanza mwezi fulani.”[2]

[1] Ibn Hibbaan (888) na ad-Daarimiy (1/428). Swahiyh kupitia zingine kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib” (132).

[2] Abu Daawuud (5092). Cheni ya wapokezi ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (5092).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 322
  • Imechapishwa: 09/09/2025