´Ubaadah bin as-Swaamit (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kuamka usiku na akasema:
لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ الْحَمْدُ لِلَّهِ وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّه العلىِّ العَظىم
“Hapana mungu mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah, Mmoja asiyekuwa na mshirika. Ana ufalme na himdi na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. Himdi zote ni za Allaah. Ametakasika Allaah. Hapana mungu mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah. Allaah ni Mkubwa. Hapana mabadiliko wala uwezo isipokuwa kwa msaada wa Allaah, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima na Mwenye hekima wa yote daima.”
Halafu akasema:
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي
“Ee Allaah! Nisamehe”
au akaomba du´aa, huitikiwa. Akitawadha na kuswali, basi swalah yake hukubaliwa.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy.
at-Tirmidhiy ameeleza ya kwamba Abu Umaamah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Anayelala kitandani mwake hali ya kuwa ni mwenye twahara na akamdhukuru Allaah (Ta´ala) mpaka pale anaposinzia hatojigeuza wakati hata mmoja usiku akimuomba Allaah kitu cha kheri duniani na Aakhirah isipokuwa Allaah atampa nacho.”[2]
Hadiyth ni nzuri.
´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:
”Alikuwua Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaposhtuka usiku husema:
لا إلهَ إِلاَّ أنْتَ سُبْحانَكَ اللَّهُمَّ، أسْتَغْفِرُكَ لِذَنْبِي، وأسألُكَ رَحْمَتَكَ، اللَّهُمَّ زِدْنِي عِلْماً وَلاَ تُزِغْ قَلْبِي بعد إذْ هَدَيْتَني وَهَبْ لِي مِنْ لَدُنْكَ رَحْمَةً، إنَّكَ أنْتَ الوَهَّابُ
“Hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe. Umetakasika kutokana na mapungufu. Ee Allaah, nakuomba msamaha kwa madhambi yangu na nakuomba rehema Zako. Ee Allaah, nizidishie elimu na usiupotoshe moyo wangu baada ya kuuongoza Nipe rehema kutoka Kwako, kwani Wewe ndiye Mpaji!”[3]
Ameipokea Abu Daawuud katika ”as-Sunan”.
[1] al-Bukhaariy (1154).
[2] at-Tirmidhiy (3526), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na ngeni.
[3] Abu Daawuud (5061) na al-Haakim (1/540), ambaye amesema kuwa cheni ya wapokezi ni Swahiyh. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (5061).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 254-255
- Imechapishwa: 22/09/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 254-255
Imechapishwa: 22/09/2025
https://firqatunnajia.com/unapoamka-usiku-unaposhtuka/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket