Umbali ambao mswalji anaweka Sutrah

Swali: Kuweka Sutrah kwa nia kwa namna ya kuweka uzi ulioko msikitini au ule ulioko kwenye mazulia kuwa ndio Sutrah yako?

Jibu: Hapana, unapaswa kuweka kijiti, kiti au kitu chochote. Uzi hautoshi. Wewe kuchora mstari ardhini, mstari unaoonekana kwa watu ardhini – kwenye mchanga au kwenye vumbi – haufai kama Sutrah.

Swali: Je, Sutrah iwe umbali wa dhiraa tatu[1] kutoka mguu wa anayeswali?

Jibu: Ndiyo, kutoka kwenye mguu wake. Kwa maana ya nyayo yake.

[1] Tazama https://sw.wikipedia.org/wiki/Dhiraa

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28935/مقدار-السترة-للمصلي-وحكم-اتخاذها-بالخطوط
  • Imechapishwa: 13/05/2025