Uliza yale yanayokuhusu na unayoyahitajia

Swali: Ni ipi hukumu ya kuuliza matukio kabla ya kutokea kwake?

Jibu: Ikiwa yanamuhusu na kwa ajili hiyo anachela juu yake ayaulize. Makatazo yalikuwa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hii leo mambo yamethibiti na hivyo mtu aulize yale anayoyahitajia. Lakini katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imekatazwa:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ

“Enyi mlioamini! Msiulizie mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni.” (05:101)

Akae kimya isipokuwa kuuliza yale yanayomuhusu. Kuhusu leo Shari´ah imeshathibiti. Mambo ya wajibu na mambo ya haramu yameshathibiti. Kwa hivyo hapana vibaya akiuliza kuhusu yale mambo anayochelea kuyaingia au yale mambo ya wajibu ambayo yamejificha kwake, kwani Shari´ah imeshathibiti.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah (09)
  • Imechapishwa: 05/11/2024