Ulipaji wa swalah kwa mwendawazimu na aliyezimia

Swali: Mwendawazimu na aliyezimia akipata fahamu baada ya muda wa swalah kuisha – je watalipa swalah?

Jibu: Mwendawazimu hapana, si mwenye kuwajibika kufanya ´ibaadah. Akiwa amepatwa na wazimu kabla ya muda wa swalah kuingia, basi jukumu la ´ibaadah limemwondokea. Lakini aliyelala atalipa, na aliyezimia anafanana na aliyelala. Akiamka atalipa katika siku moja, mbili au tatu, kama ilivyopokelewa kutoka kwa ´Ammaar bin Yaasir (Radhiya Allaahu ´anh) na wengineo. Baadhi ya wanazuoni wamesema kwamba akizimia siku nzima kamili hatolipa, lakini ikiwa ni chini ya siku basi atalipa. Lililo karibu zaidi na usawa – Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba anafanana na aliyelala. Ikiwa ni siku moja, mbili au tatu atalipa, na ikiwa ni zaidi hatalipa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31124/حكم-قضاء-الصلاة-للمجنون-والمغمى-عليه
  • Imechapishwa: 03/10/2025