Swali: Mwanamke alipatwa na maradhi ya shinikizo la damu ghafla na sukari pia ikapanda. Akabaki hospitalini takriban siku tatu akiwa hajitambui. Kisha akatoka hospitali na bado hawezi kuswali zile swalah zilizompita hadi zikapita siku kumi. Anataka sasa kulipa swalah alizokosa, lakini hawezi kuziswali ipasavyo. Hivyo inawalazimu wanawe kumwelekeza ndani ya swalah, kwa namna ya kwamba wanamwambia muda wa kurukuu na kusujudu. Jengine ni kwamba akiwa ndani ya swalah hajui ameswali Rak´ah ngapi. Je, analazimika kulipa swalah alizokosa katika hali hii au hapana?
Jibu: Muda wa kuwa akili yake imeharibika, hakuna kitu kinachomlazimu. Ikiwa akili yake bado haipo imerudi kwa muda wa siku tatu, basi sahihi ni kwamba mpaka umewekwa ni muda wa siku tatu za kupoteza fahamu. Baadhi ya wanazuoni wamesema mpaka uliyowekwa ni mchana mmoja na usiku wake tu. Akizidi hapo basi hukumu yake ni hukumu ya mwendawazimu. Ama ikishakuwa siku tatu basi salama zaidi ni yeye kulipa, kama inavyosimuliwa kuwa ´Ammaar alipoteza fahamu siku tatu na akalipa. Ama huyu, ikiwa akili yake ilirudi baada ya siku tatu, atalipa hizo siku tatu. Lakini akibakia siku kumi bila kujua kuswali, basi hakuna kulipa juu yake.
Swali: Lakini hali yake ni kuwa anapomaliza swalah hajui ameswali ngapi na hajui kitu?
Jibu: Hii maana yake ni kuwa akili yake bado haijamrudia, bado yuko katika hali ya kupoteza fahamu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31078/ما-حكم-قضاء-الصلاة-لمن-زال-عقله-عدة-ايام
- Imechapishwa: 01/10/2025
Swali: Mwanamke alipatwa na maradhi ya shinikizo la damu ghafla na sukari pia ikapanda. Akabaki hospitalini takriban siku tatu akiwa hajitambui. Kisha akatoka hospitali na bado hawezi kuswali zile swalah zilizompita hadi zikapita siku kumi. Anataka sasa kulipa swalah alizokosa, lakini hawezi kuziswali ipasavyo. Hivyo inawalazimu wanawe kumwelekeza ndani ya swalah, kwa namna ya kwamba wanamwambia muda wa kurukuu na kusujudu. Jengine ni kwamba akiwa ndani ya swalah hajui ameswali Rak´ah ngapi. Je, analazimika kulipa swalah alizokosa katika hali hii au hapana?
Jibu: Muda wa kuwa akili yake imeharibika, hakuna kitu kinachomlazimu. Ikiwa akili yake bado haipo imerudi kwa muda wa siku tatu, basi sahihi ni kwamba mpaka umewekwa ni muda wa siku tatu za kupoteza fahamu. Baadhi ya wanazuoni wamesema mpaka uliyowekwa ni mchana mmoja na usiku wake tu. Akizidi hapo basi hukumu yake ni hukumu ya mwendawazimu. Ama ikishakuwa siku tatu basi salama zaidi ni yeye kulipa, kama inavyosimuliwa kuwa ´Ammaar alipoteza fahamu siku tatu na akalipa. Ama huyu, ikiwa akili yake ilirudi baada ya siku tatu, atalipa hizo siku tatu. Lakini akibakia siku kumi bila kujua kuswali, basi hakuna kulipa juu yake.
Swali: Lakini hali yake ni kuwa anapomaliza swalah hajui ameswali ngapi na hajui kitu?
Jibu: Hii maana yake ni kuwa akili yake bado haijamrudia, bado yuko katika hali ya kupoteza fahamu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31078/ما-حكم-قضاء-الصلاة-لمن-زال-عقله-عدة-ايام
Imechapishwa: 01/10/2025
https://firqatunnajia.com/ulipaji-wa-swalah-kwa-aliyepoteza-fahamu-kwa-siku-nyingi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket