Swali: Ni ipi hukumu ya kulingania kwa Allaah kwa mpangilio?

Jibu: Mpangilio ambao hauendi kinyume na Qur-aan na Sunnah ni jambo linalotakikana. Ni lazima kupangilia. Lakini watu hawa wanatumia vibaya kwa ajili ya kupitisha uvyama. Kuhusu mpangilio ndani ya mipaka ya Qur-aan na Sunnah ni jambo lisilokuwa na budi.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 403
  • Imechapishwa: 10/07/2025