Swali: Hakika anayezingatia juhudi zenu njema basi hawezi kusema jengine isipokuwa kukuombeeni du´aa Allaah awalipeni kheri nyingi wewe na Mashaykh wengine wote mnaojitolea kwa elimu na kuifundisha. Mnajua ubora wenu kwamba nchi yetu inaleta wafanyakazi kutoka mataifa mbalimbali na mnajua kuwa wengi wao si waislamu. Tumewaandalia nini hawa katika nasaha, ulingano na uongofu? Pamoja na swali hili, linanijia wazo la pendekezo ambalo naona lifanywe – Allaah anajua kuwa mimi ni mwenye kuwatakia kheri – je, mnaonaje tukileta watafsiri wa lugha zote zilizopo kwetu nikimaanisha wafanyakazi waliopo kwetu na tukawaleta watafsiri wa kuwatafsiria, kisha Mashaykh wetu wakatoa mihadhara na kuwafahamisha Uislamu katika maeneo yao? Kwa sababu wengi wao hawajui kuhusu Uislamu isipokuwa kwa jina tu. Ni kwa nini basi tusitumie fursa hii ikiwa ni lazima kuwaleta hawa washirikina au watu wa dini nyingine, basi ni lazima kuwe na juhudi kutoka kwetu za kuwalingania hawa na kwa sababu Allaah akikuongozea mtu mmoja kupitia wewe ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.
Jibu: Hili lipo tayari, ee muulizaji. Kwa hakika tumeandaa kwa hilo yale yanayohitajika na tumesisitiza kwa walinganiaji na umewekwa mpango katika nchi yote wa kuwalingania, kuwaongoza kwenye kheri kupitia watafsiri na pia vitabu vilivyotafsiriwa vinagawiwa miongoni mwao. Tunamuomba Allaah atusaidie kufikia ukamilifu na utimilifu na alete manufaa kwa hilo na awaongoze waislamu wote na wasiokuwa waislamu kuingia katika haki na kuwa na uimara juu yake.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3259/كيفية-دعوة-العمال-غير-المسلمين
- Imechapishwa: 10/10/2026
Swali: Hakika anayezingatia juhudi zenu njema basi hawezi kusema jengine isipokuwa kukuombeeni du´aa Allaah awalipeni kheri nyingi wewe na Mashaykh wengine wote mnaojitolea kwa elimu na kuifundisha. Mnajua ubora wenu kwamba nchi yetu inaleta wafanyakazi kutoka mataifa mbalimbali na mnajua kuwa wengi wao si waislamu. Tumewaandalia nini hawa katika nasaha, ulingano na uongofu? Pamoja na swali hili, linanijia wazo la pendekezo ambalo naona lifanywe – Allaah anajua kuwa mimi ni mwenye kuwatakia kheri – je, mnaonaje tukileta watafsiri wa lugha zote zilizopo kwetu nikimaanisha wafanyakazi waliopo kwetu na tukawaleta watafsiri wa kuwatafsiria, kisha Mashaykh wetu wakatoa mihadhara na kuwafahamisha Uislamu katika maeneo yao? Kwa sababu wengi wao hawajui kuhusu Uislamu isipokuwa kwa jina tu. Ni kwa nini basi tusitumie fursa hii ikiwa ni lazima kuwaleta hawa washirikina au watu wa dini nyingine, basi ni lazima kuwe na juhudi kutoka kwetu za kuwalingania hawa na kwa sababu Allaah akikuongozea mtu mmoja kupitia wewe ni bora kwako kuliko ngamia wekundu.
Jibu: Hili lipo tayari, ee muulizaji. Kwa hakika tumeandaa kwa hilo yale yanayohitajika na tumesisitiza kwa walinganiaji na umewekwa mpango katika nchi yote wa kuwalingania, kuwaongoza kwenye kheri kupitia watafsiri na pia vitabu vilivyotafsiriwa vinagawiwa miongoni mwao. Tunamuomba Allaah atusaidie kufikia ukamilifu na utimilifu na alete manufaa kwa hilo na awaongoze waislamu wote na wasiokuwa waislamu kuingia katika haki na kuwa na uimara juu yake.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3259/كيفية-دعوة-العمال-غير-المسلمين
Imechapishwa: 10/10/2026
https://firqatunnajia.com/ulinganizi-kwa-wafanyakazi-wasio-waislamu/