Swali: Kati yangu na ndugu yangu kuna ugomvi kuhusu kuleta waimbaji wanawake katika harusi yetu. Hoja yake ni kwamba hii ni katika kuitangaza ndoa ilihali jambo hilo liko mbali na Sunnah. Mnajua yale yanayoambatana na waimbaji hao kama nyimbo chafu, kuchanganyika kwa wanaume na wanawake, kupiga picha na mengineyo. Tunaomba mubainishe haki na mtupatanishe na Allaah awalipe kheri nyingi.
Jibu: Kilichosuniwa katika ndoa ni kuitangaza na kuidhihirisha. Aidha kuwepo tangazo lake kwa namna ambayo wanawake wanakusanyika peke yao na wanaume wanakusanyika peke yao, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha kuitangaza ndoa. Ilikuwa ikifanywa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba wanawake hukusanyika kwa watu wa bibi harusi, kisha wanamsindikiza kwenda kwa mume wake na miongoni mwao kunakuwa na baadhi ya nyimbo za kawaida zisizo na ubaya, za kumpongeza mume, watu wa mume, kumpongeza bibi harusi na watu wake na mfano wa hayo. Kama mfano wa kusema:
Tumekujieni, tumekujieni
tupokeeni tukusalimieni
Hili halina ubaya. Ama nyimbo za maovu ambazo ndani yake kuna kusifu pombe, wito wa mapenzi ya wanawake au wanaume au kuinua sauti kwa vipaza sauti, basi yote hayo ni maovu. Ama kuimba kwa kawaida kati ya wanawake peke yao bila kuchanganyika na wanaume na katika sehemu yao, bila vipaza sauti na bila mchanganyiko, basi hilo halina ubaya. Hilo ni katika kuitangaza ndoa, kama ilivyokuwa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wake wa Mtume walikuwa wanahudhuria hilo.
Swali: Vipi wanaume?
Jibu: Ama wanaume, hapana. Haijuzu kwao kuchanganyika na wanawake. Lakini wakikusanyika peke yao ambapo wakafanya mambo kama kurusha silaha, kusoma mashairi ya kiarabu yasiyo na ubaya, bila ngoma wala mambo mabaya, basi hakuna ubaya. Wafanye hivyo wakiwa mbali na wanawake. Ni kama wanavyofanya baadhi ya watu, wakirusha silaha wakati wa harusi kwa ajili ya kutangaza ndoa, kukusanyika juu ya mashairi mazuri yenye hamasa, yanayohimiza maadili mema, matendo mazuri na ushujaa na kujifunza kutumia silaha, hatuoni ubaya katika hilo. Kwa hakika wahabeshi walifanya hivyo katika msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Walikuwa wakicheza kwa mikuki na Mtume akawaangalia. Hili halina ubaya, kama alivyolikubali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ikiwa ni katika mambo ya kujifunza masuala ya kivita, jinsi ya kurusha mkuki, kubeba silaha, kutumia bunduki, upanga na mfano wa hayo. Ama ikiwa kuna kuchanganyika kwa wanaume na wanawake, kuwepo ngoma au nyimbo za maovu zinazohusiana na wanawake, uzuri wao, mwito wa maasi na uasi, pombe na mambo kama hayo, basi hayo yanakatazwa na yanapaswa kuzuiwa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3272/حكم-احضار-المغنيات-بحجة-اعلان-النكاح
- Imechapishwa: 10/10/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3272/حكم-احضار-المغنيات-بحجة-اعلان-النكاح
Imechapishwa: 10/10/2026
https://firqatunnajia.com/ndoa-haitangazwi-kwa-nyimbo-za-kihuni/