Swali: Anashughulishwa na kumhudumia mama yake na kumtunza, kiasi kwamba anashindwa kutoka pamoja na ndugu zake wema, khaswa siku ya darsa hili ili kulihudhuria na kulisikiliza na hivyo anakosa kheri nyingi pamoja na hili. Unasemaje juu ya hili?
Jibu: Kutafuta elimu ni wajibu ikiwa mtu ana haja nayo, kutafuta elimu ni wajibu. Ikiwa wazazi wake wanakataa, basi hakuna ubaya kuwaasi katika hilo kwa ajili ya kutafuta elimu ya wajibu. Kwa sababu elimu ni jambo ambalo mja ana dharurah nalo. Lakini hilo lifanyike kwa mtindo mzuri, kwa maneno mazuri, aombe radhi na ruhusa na amweleweshe kuwa ni mwenye kuhitaji kutafuta elimu. Hivyo atoke kwenda kutafuta elimu kama kuhudhuria darsa hii au kuhudhuria vikao vya elimu. Lakini afanye hivo kwa njia nzuri na mtindo mzuri. Ikiwa wazazi wake wanamhitaji na anaweza kumweka mtu wa kumwakilisha katika muda ule anaotoka ili kuwahudumia mahitaji yao, basi hilo ndilo linalopaswa. Ni lazima afanye kila analoweza katika kuwafanyia wema, pamoja na kuwa na bidii katika kutafuta elimu. Kadhalika ikiwa wanamzuia kuswali kwa mkusanyiko, basi anapaswa kuswali kwa mkusanyiko na wala asiwatii katika hilo. Vivyo hivyo ikiwa wanamzuia kutekeleza wajibu ulio juu yake kama kutoa zakaah au kufunga Ramadhaan, basi hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba. Hakika hapana vyenginevyo utiifu ni katika mambo ya kheri tu, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Lakini yote yafanyike kwa mtindo mzuri, si kwa ukali wala nguvu. Awaeleze, awatafutie radhi na azungumze nao kwa maneno mazuri, huenda Allaah (Ta´ala) akawaongoza ili kusiwe na chuki baina yao.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3278/انشغال-الابن-برعاية-امه-عن-طلب-العلم
- Imechapishwa: 10/10/2026
Swali: Anashughulishwa na kumhudumia mama yake na kumtunza, kiasi kwamba anashindwa kutoka pamoja na ndugu zake wema, khaswa siku ya darsa hili ili kulihudhuria na kulisikiliza na hivyo anakosa kheri nyingi pamoja na hili. Unasemaje juu ya hili?
Jibu: Kutafuta elimu ni wajibu ikiwa mtu ana haja nayo, kutafuta elimu ni wajibu. Ikiwa wazazi wake wanakataa, basi hakuna ubaya kuwaasi katika hilo kwa ajili ya kutafuta elimu ya wajibu. Kwa sababu elimu ni jambo ambalo mja ana dharurah nalo. Lakini hilo lifanyike kwa mtindo mzuri, kwa maneno mazuri, aombe radhi na ruhusa na amweleweshe kuwa ni mwenye kuhitaji kutafuta elimu. Hivyo atoke kwenda kutafuta elimu kama kuhudhuria darsa hii au kuhudhuria vikao vya elimu. Lakini afanye hivo kwa njia nzuri na mtindo mzuri. Ikiwa wazazi wake wanamhitaji na anaweza kumweka mtu wa kumwakilisha katika muda ule anaotoka ili kuwahudumia mahitaji yao, basi hilo ndilo linalopaswa. Ni lazima afanye kila analoweza katika kuwafanyia wema, pamoja na kuwa na bidii katika kutafuta elimu. Kadhalika ikiwa wanamzuia kuswali kwa mkusanyiko, basi anapaswa kuswali kwa mkusanyiko na wala asiwatii katika hilo. Vivyo hivyo ikiwa wanamzuia kutekeleza wajibu ulio juu yake kama kutoa zakaah au kufunga Ramadhaan, basi hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba. Hakika hapana vyenginevyo utiifu ni katika mambo ya kheri tu, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Lakini yote yafanyike kwa mtindo mzuri, si kwa ukali wala nguvu. Awaeleze, awatafutie radhi na azungumze nao kwa maneno mazuri, huenda Allaah (Ta´ala) akawaongoza ili kusiwe na chuki baina yao.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3278/انشغال-الابن-برعاية-امه-عن-طلب-العلم
Imechapishwa: 10/10/2026
https://firqatunnajia.com/kumhudumia-mama-yake-kunamshughulisha-na-kutafuta-elimu/