Anaposimama kwa ajili ya swalah aseme:
الله أكبر
“Allaah ni mkubwa.”
Imamu huitamka Takbiyr hii na Takbiyr nyingine zote kwa sauti ya juu ili wale walio nyuma yake wasikie. Wengine huitamka kwa sauti ya chini.
Huinua mikono yake wakati wa kuanza Takbiyr mpaka usawa wa mabega yake au ncha za masikio yake. Huweka mikono yake chini ya kitovu chake, huweka macho yake kwenye sehemu yake ya kusujudia. Kisha husema:
سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ وتَبَارَكَ اسْمُكَ وَتَعَالى جَدُّكَ وَلا إِله غَيْرُكَ
“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah, kutokamana na kasoro zote na himdi zote ni Zako. Limetukuka jina Lako, ufalme Wako ni mkubwa na hapana mungu wa haki mwengine asiyekuwa Wewe.”[1]
Kisha husema:
أعوذ بالله من الشيطان الرجيم
“Najilinda kwa Allaah kutokana na shaytwaan aliyefukuzwa mbali.”
Kisha husema:
بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
“Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.”
Wala asiseme kwa sauti ya juu chochote katika hayo. Anas amesema:
“Niliswali nyuma ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan – na sikumsikia yeyote miongoni mwao akiseme kwa sauti kubwa:
بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ
“Kwa jina la Allaah, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu.”[2]
Halafu husoma al-Faatihah, kwa sababu hakuna swalah kwa yule asiyeisoma, isipokuwa maamuma – kwa sababu kisomo cha imamu kinamtosheleza. Hata hivyo inapendekezwa asome katika nyakati ambazo imamu amenyamaza na katika swalah ambazo anasoma kimyakimya.
Baada ya hapo asome Suurah nyingine. Ikiwa swalah ni Fajr, basi asome Suurah katika zile ndefu za Mufasswal. Ikiwa ni swalah ya Maghrib, asome miongoni mwa fupi zake. Katika swalah nyingine asome Suurah miongoni mwa za kati yake.
Imamu asome kwa sauti kubwa katika Fajr. Afanye vivyo hivyo katika zile Rak´ah mbili za mwanzo za Maghrib na ´Ishaa. Atasoma kimyakimya katika Rak´ah zilizosalia.
Kisha alete Takbiyr, ainue mikono yake – kama alivyoinua katika ile Takbiyr ya kwanza – kisha aende katika Rukuu´.
Kisha aweke mikono yake juu ya magoti yake, aachanishe vidole vyake, anyooshe mgongo wake, aweke kichwa chake katika usawa wake na aseme:
سبحان ربي العظيم
“Ametakasika Mola wangu aliyetukuka.”
Kisha huinua kichwa chake huku akisema:
سَمعَ الله لِمنْ حَمِدَه
“Allaah amemsikia mwenye kumuhimidi.”
na huinua mikono yake kama alivyoinua mara ya kwanza. Anaponyooka sawasawa husema:
رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ مِلءَ السَّمَواتِ وَمِلْءَ الأَرْضِ وَمِلءَ مَا بَيْنَهُمَا وَمِلْءَ مَا شِئْتَ مِنْ شَيْءٍ بَعْد
“Mola wetu! Himdi zote ni Zako zimejaa mbingu, ardhi na vyengine vyote Ulivyovitaka baada yake.”
Maamuma afupishe kwa kusema:
رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ
“Mola wetu! Himdi zote ni Zako!”
Kisha alete Takbiyr – bila kuinua mikono yake kama alivyofanya mara ya kwanza – kisha aende katika Sujuud. Iwe cha kwanza kinachogusa ardhi ni magoti yake, kisha viganja vyake, kisha paji la uso wake na pua yake. Huweka mikono yake mbali na mbavu zake na tumbo lake mbali na mapaja yake. Huweka mikono yake usawa wa mabega yake, na huwa juu ya ncha za vidole vya miguu yake. Kisha husema mara tatu:
سبحان ربي الأعلى
“Ametakasika Mola wangu Aliye juu kabisa.”
Kisha huleta Takbiyr, akiinua kichwa chake na hukaa kwa kukunjua mguu wa kushoto na kukalia, huku akiunyanyua mguu wa kulia na kukunja vidole vyake kuelekea Qiblah, na husema mara tatu:
رَبِّ اغْفِرْ لِي
“Mola! Nisamehe!”
Kisha husujudu mara ya pili kama alivyofanya mara ya kwanza.
Kisha huleta Takbiyr, akainuka juu na kuswali Rak´ah ya pili kama alivyofanya katika ile ya kwanza.
Anapomaliza Rak´ah mbili, hukaa kwa ajili ya Tashahhud akiwa amekalia mguu wa kushoto. Huweka mkono wake wa kushoto juu ya paja lake la kushoto na mkono wake wa kulia juu ya paja lake la kulia. Hukunja kidole kidogo na kidole cha pete, huunganisha kidole gumba na cha kati kwa kutengeneza duara na huashiria kwa kidole cha shahaadah katika Tashahhud yake mara kadhaa na kusema:
التحيات لله، و الصلوات و الطيبات، السلام عليك أيها النبي و رحمة الله و بركاته، السلام علينا و على عباد الله الصالحين، أشهد أن لا إله إلا الله و أشهد أن محمداً عبده و رسوله
“Maadhimisho, swalah na mazuri yote yanamstahikia Allaah. Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee Mtume! Amani ishuke juu yetu na juu ya waja wema wa Allaah. Nashuhudia ya kwamba hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja na Mtume Wake.”[3]
Hii ndiyo sahihi zaidi katika yaliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu Tashahhud. Kisha husema:
اللهم صل على محمد و على آل محمد كما صليت على إبراهيم و على آل إبراهيم، إنك حميد مجيد. اللهم بارك على محمد و على آل محمد كما باركت على إبراهيم و على آل إبراهيم، إنك حميد مجيد
“Ee Allaah! Msifu Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyomsifu Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa. Ee Allaah! Mbariki Muhammad, jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na jamaa zake Ibraahiym. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kuhidimiwa na Mwenye kutukuzwa.”
Vilevile inapendekezwa ajikinge kutokana na adhabu ya Moto, adhabu ya kaburi, fitina ya uhai na kifo na fitina ya al-Masiyh ad-Dajjaal.
Kisha hutoa salamu upande wake wa kulia kwa kusema:
السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللهِ
”Amani na rehema za Allaah ziwe juu yenu.”
Afanye vivyo hivyo upande wake wa kushoto.
Ikiwa swalah ni zaidi ya Rak´ah mbili, husimama baada ya Tashahhud ya kwanza kama anavyosimama kutoka katika kusujudu. Kisha huswali Rak´ah mbili bila ya kusoma chochote katika hizo baada ya al-Faatihah. Anapokaa katika Tashahhud ya mwisho, basi hukaa mkao wa Tawarruk kwa namna ya kwamba husimamisha mguu wake wa kulia, kuufanya mguu wake wa kushoto ulale na kuutoa upande wake wa kulia. Hafanyi Tawarruk isipokuwa kwenye Tashahhud yake ya mwisho katika ile swalah yenye Tashahhud mbili.
Anapotoa Tasliym, humwomba Allaah msamaha mara tatu na husema:
اللَّهُمَّ أَنْتَ السَّلاَمُ وَمِنْك السَّلاَمُ تَبَارَكْتَ يَا ذَا الْجَلاَلِ وَالإِكْرام
“Ee Allaah! Hakika Wewe ni mkamilifu usiyokuwa na mapungufu na amani inatoka Kwako. Umetukuka, ee Mwenye utukufu na ukarimu.”
[1] Abu Daawuud (775), at-Tirmidhiy (243) na Ibn Maajah (806). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (3/361).
[2] Muslim (399).
[3] al-Bukhaariy (835) na Muslim (402).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 24-25
- Imechapishwa: 10/10/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 24-25
Imechapishwa: 10/10/2026
https://firqatunnajia.com/20-namna-ya-swalah/