Ulazima wa mahari mapya wakati wa kumrejea mke baada ya eda kumalizika

Swali: Je, ni lazima kutoa mahari mapya katika zile sura na hali ambazo mume amelazimika kumrejea mkewe kwa kufunga ndoa mpya?

Jibu: Ndio, ni lazima kufunga ndoa mpya. Ni lazima kutoa mahari mengine hata kama watafunga ndoa mpya. Haijalishi kitu ijapo mahari yatakuwa kidogo:

”Hakuna ndoa isipokuwa kwa mahari.”

أَن تَبْتَغُوا بِأَمْوَالِكُم

”… mtafute [kuwaoa] kwa mali zenu… ”[1]

[1] 04:24

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25203/حكم-المهر-اذا-رجع-الزوج-الى-زوجته-بعقد-جديد
  • Imechapishwa: 21/02/2025