Swali: Kujifunza visomo saba ni faradhi kwa baadhi ya watu?

Jibu: Tukitaja maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Qur-aan imeteremshwa kwa herufi saba.”[1]

basi kutambua herufi saba ni miongoni mwa faradhi kwa baadhi ya watu.

Swali: Mpaka kwa wanawake pia?

Jibu:

”Hakika si venginevyo wanawake ni ndugu zake wanamme.”[2]

Swali: Kwa hiyo ni lazima kuwepo kikosi  cha wanawake kinachojifunza visomo?

Jibu: Ndio.

[1] Ahmad (1495).

[2] Ahmad. Tazama ”as-Swahiyhah” (2863).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 58-59
  • Imechapishwa: 01/07/2022