Ukweli kuhusu sindano ya lishe kwa mfungaji

Swali: Nimesoma katika baadhi ya vitabu vya Fiqh kukiwemo kitabu “Fiqh-us-Sunah” cha mtunzi Shaykh Sayyid Saabiq ya kwamba sindano za lishe na nyenginezo ambazo haziingii kupitia njia ya tumbo au mdomo kwamba hazifunguzi.  Natambua kuwa kuna maoni ya baadhi ya wanachuoni ambao wanahukumu kinyume na hivo. Ni yepi maoni yanayotambulika kwa wanachuoni wengi?

Jibu: Sahihi ni kwamba sindano ya lishe inamfunguza mfungaji pale atapoitumia kwa kukusudia. Ama kuhusu sindano za kawaida hazimfunguzi yule mwenye kufunga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/257-258 )
  • Imechapishwa: 26/05/2018