Swali: Je, inazingatiwa ni Sunnah kuondoka baada ya chakula katika karamu ya ndoa au mnasaba mwingine?

Jibu: Hii ndio Sunnah:

فَإِذَا طَعِمْتُمْ فَانتَشِرُوا وَلَا مُسْتَأْنِسِينَ لِحَدِيثٍ

”Mkimaliza kula, basi sambaeni na wala msikae kujifariji kwa mazungumzo.”[1]

Asiwaudhi. Asiwaudhi watu wa nyumbani. Akimaliza kula aondoke zake. Isipokuwa kulingana na desturi ikiwa kuna salio kama vile kahawa, chai au manukato. Italingana na mila na hapo hakuna neno. Kwa sababu ni jambo linaloandama chakula.

Swali: Aayah ni yenye kuenea?

Jibu: Ni yenye kuenea.

[1] 33:53

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23858/متى-يكون-الانصراف-بعد-اجابة-الدعوة
  • Imechapishwa: 20/05/2024