Swali 898: Mwanaume akimwambia mke wake “ukifanya jambo fulani basi wewe ni kama mama au dada yangu” ambapo baadaye mke akafanya jambo lile kwa kusahau.

Jibu: Ni lazima kwake kukafiri kafara ya yamini. Kama hakusahau basi amemfananisha mkewe na mama yake. Kwa sababu watu wamepewa udhuru:

رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]

[1] 02:286

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Mar´ah al-Muslimah, uk. 359
  • Imechapishwa: 27/03/2020