Swali: Tunaona baadhi ya wenye ulinganizi wanaolingania watu wanakwenda kinyume na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kunyoa ndevu. Je, inajuzu kwa walinganizi kufanya hivyo?
Jibu: Ni wajibu kwa walinganizi wasio walinganizi kuziacha ndevu, kuzijaza, kuziachia na kutoziharibu kwa kunyoa au kuzifupisha. Hivi ndivyo alivyowaamuru Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Kateni masharubu na achieni ndevu. Nendeni kinyume na washirikina.”
”Fupisheni masharubu na achieni ndevu. Nendeni kinyume na waabudia moto.”
Kwa hiyo alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwaamuru kuziacha ndevu na kuzijaza. Aidha alikuwa anakataza kuzikata na kuzinyoa. Kuzinyoa ni vibaya zaidi na ni haramu zaidi. Kuzinyoa ni jambo baya zaidi kuliko kuzifupisha, ingawa yote mawili ni haramu. Kwa walinganizi ni jambo baya zaidi, kwa sababu wao ni walinganizi. Wajibu kwao ni mkubwa zaidi. Mwanafunzi dhambi juu yake huwa kubwa zaidi kuliko mtu wa kawaida, ijapokuwa wote wanaingia katika dhambi wanapofanya kile ambacho Allaah amekiharamisha. Lakini kuchukua kutoka katika ndevu kwa mwanafunzi au kuzikata dhambi yake huwa kubwa zaidi kwa sababu yeye ni kigezo.
Mwanafunzi: Wanasema kuwa Sunnah mtu haadhibiwi juu yake. Wanaona ni Sunnah tu.
Ibn Baaz: Kusema kwamba ni Sunnah tu ni kosa. Bali ni wajibu. Sunnah kwa maana ya njia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini ni wajibu. Anaingia katika dhambi mwenye kuiacha. Kisha tukikadiria kwamba ingekuwa ni jambo la kupendekezwa tu, haikufaa kwa walinganizi na wanafunzi kuacha Sunnah ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alidumu juu yake, akaiamuru na akalingania kwayo. Tusemeje ilihali uhalisia wa mambo ni kinyume na hivo?
Msingi katika maamrisho ni wajibu na msingi katika makatazo ni uharamu. Hakuna kitu kinachoonyesha kinyume. Wala hakuhifadhiwa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alizinyoa au kuzikata hadi ikaambiwa kuwa amri hiyo si ya wajibu hali ya kuwa kitendo chake kinaonyesha kutokuwa wajibu. Alipoamuru kuziacha na kuziachia yeye na Maswahabah wake wakaziacha, hilo linaonyesha kuwa ni wajibu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/984/هل-يجوز-للدعاة-حلق-او-تقصير-اللحية
- Imechapishwa: 01/01/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/984/هل-يجوز-للدعاة-حلق-او-تقصير-اللحية
Imechapishwa: 01/01/2026
https://firqatunnajia.com/ujumbe-kwa-walinganizi-na-wanafunzi-wenye-kunyoa-na-kukata-ndevu/