Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

126 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameelezakuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

 بَينَما رَجُلٌ يَمشي بِطَريقٍ اشْتَدَّ عَلَيهِ العَطَشُ، فَوَجَدَ بِئرًا فَنَزَلَ فِيهَا فَشربَ، ثُمَّ خَرَجَ فإذَا كَلْبٌ يَلْهَثُ يأكُلُ الثَّرَى مِنَ العَطَشِ، فَقَالَ الرَّجُلُ: لَقَدْ بَلَغَ هَذَا الكَلْبُ مِنَ العَطَشِ مِثلُ الَّذِي كَانَ قَدْ بَلَغَ مِنِّي فَنَزَلَ البِئْرَ فَمَلأَ خُفَّهُ مَاءً ثُمَّ أمْسَكَهُ بفيهِ حَتَّى رَقِيَ، فَسَقَى الكَلْبَ، فَشَكَرَ الله لَهُ، فَغَفَرَ لَهُ. قالوا: يَا رَسُول اللهِ، إنَّ لَنَا في البَهَائِمِ أَجْرًا؟ فقَالَ: في كُلِّ كَبِدٍ رَطْبَةٍ أجْرٌ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية للبخاري: فَشَكَرَ اللهُ لَهُ، فَغَفَرَ لَهُ، فأدْخَلَهُ الجَنَّةَ

“Kulikuwa na mtu aliyekuwa akitembea na ghafla akashikwa na kiu ambapo akaona kisima na akawa ameteremka na kunywa maji. Alipokuwa anatoka kwenye kisima kile akaona mbwa yuwahema na huku anakula udongo kutokana na kiu. Yule mtu akasema mbwa huyu ameshikwa na kiu kama nilichokuwa nacho. Akateremka kwenye kisima na kujaza soksi yake maji na huku ameyazuia na mdomo wake na kwenda kwa yule mbwa na akamnywesha. Yule mbwa akamshukuru na hiyo ndio ikawa sababu ya Allaah kumsamehe.” Wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Kwani sisi tuna ujira kwa wanyama?” Akasema: “Kuna ujira kwa kunywesha kila kilicho hai.”[1]

Katika upokezi wa al-Bukhaariy imekuja:

“Allaah akamshukuru kwa hilo na akamwingiza Peponi.”

Hili linathibitisha maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Pepo iko karibu zaidi na mmoja wenu kuliko kamba za viatu vyake. Na Moto ni vivyo hivyo.”

Kitendo kidogo Allaah amemshukuru kwacho mtendaji na akamsamehe madhambi yake na kumwingiza Peponi.

[1] al-Bukhaariy na Muslim

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/171-172)
  • Imechapishwa: 02/06/2024