Swali: Inasemekana kwamba kutokausha au kufuta maji baada ya kumaliza kutawadha kwa kitambaa, leso au kitu kama hicho ni Sunnah. Vivyo hivyo kabla ya kuanza kula kwa mkono baada ya kuosha mikono miwili?

Jibu: Kutokausha au kutofuta maji yaliyobaki mikononi baada ya wudhuu´, kabla ya kula au baada ya kula, si Sunnah. Bali katika mambo yote hayo mtu yuko huru; akitaka anaweza kuyafuta na akitaka anaweza kuyaacha.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/239)
  • Imechapishwa: 06/11/2026