Ufutaji kwenye soksi yenye tundu dogo upande wa chini ya mguu

Swali: Vipi ikiwa kuna tundu kwenye soksi upande wa chini ya mguu?

Jibu: Kilicho sahihi ni kwamba inasamehewa iwapo tundu hilo ni dogo. Ikiwa mtu atachukua tahadhari na kulishona au kulirekebisha au kuzibadilisha, itakuwa bora zaidi. Hata hivyo kilicho sahihi ni kwamba tundu dogo linalozingatiwa kuwa dogo kwa kawaida husamehewa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24736/ما-حكم-الخروق-اليسيرة-في-الجورب
  • Imechapishwa: 05/12/2024