Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninakuusieni kumcha Allaah na kusikiliza na kutii hata kama mtatawaliwa na mja wa kihabeshi.”[1]

Hili ni sawa mamlaka yake ni yenye kuenea kama mfano wa raisi mkuu wa nchi nzima; au mamlaka maalum kama mfano wa kiongozi wa mji, kiongozi wa kabila na mfano wa hao.

Wamekosea wale waliofikiria kuwa makusudio ya:

“… hata kama mtatawaliwa na mja wa kihabeshi”

kwamba ni yule mtawala mkubwa [anayewaongoza waislamu wote]. Wanachuoni wa Fiqh wanamwita. Neno “utawala” katika Shari´ah linahusu uongozi wa kiongozi mkubwa na uongozi wa viongozi wadogo kama viongozi wa miji. Dalili ya hili tangu ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) atawale waislamu walikuwa wakimwita khaliyfah “kiongozi wa waislamu” [Amiyr-ul-Mu´miniyn]. Walikuwa wakimfanya kuwa ni kiongozi jambo ambali halina shaka yoyote ndani yake. Vilevile anaitwa kiongozi “Imaam” na mfalme “Sultwaan”. Lakini mfumo wa Maswahabah walikuwa wakimwita “kiongozi wa waislamu.”

[1]Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2676) na Ibn Maajah (42).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/277)
  • Imechapishwa: 27/10/2024