Swali: Kuna mwanamke mmoja ambaye hali yake ni nzuri alishughulishwa na hakuchinja Udhhiyah isipokuwa katika tarehe 15 ya Dhul-Hijjah ndipo akachinja. Inazingatiwa kuwa ni Udhhiyah?

Jibu: Kichinjwa kilichotajwa hakiwi Udhhiyah, kwa sababu wakati wa Udhhiyah umeshaondoka kwa kuzama kwa jua ile tarehe 13 ya mwezi wa Dhul-Hijjah. Hata hivyo kinazingatiwa kuwa ni swadaqah. Ale sehemu yake na awape swadaqah mafukara. Pia awape zawadi wale majirani na jamaa atakaowataka.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/39)
  • Imechapishwa: 15/06/2024