Uchinjaji katika sikukuu zisohusiana na Uislamu

Swali: Kuchinja katika maulidi, kusherehekea usiku wa tarehe 27 Rajab, kusherehekea siku ya Hijrah, kusherehekea siku ya mama na siku ya mapinduzi ni miongoni mwa mambo kabla ya kuja Uislamu?

Jibu: Sikukuu, mbali na ´Iyd-ul-Fitwr, ´Iyd-ul-Adhwhaa, siku ya ijumaa ambayo ni sikukuu ya wiki, nyenginezo zote ni miongoni mwa mambo ya kabla ya kuja Uislamu. Kwa sababu tumetambulisha (الجاهلية) kwamba ni yale ambayo hayakutajwa ndani ya Qur-aan na Sunnah.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 466
  • Imechapishwa: 31/07/2025