Swali: Je, watu wa Jeddah wana wajibu wa kufanya Twawaaf-ul-Wadaa´ na ni ipi dalili?

Jibu: Ndio, kwa kuwa wao si miongoni mwa watu wa Haram na wala hawako katika hukumu ya watu wa Haram. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asiondoke yeyote miongoni mwenu mpaka mwisho wa kitendo chake kiwe ni kuiaga Nyumba.”

Ameipokea Muslim.

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Watu wameamrishwa mwisho wa matendo yao iwe ni kuiaga Nyumba, isipokuwa amefanyiwa wepesi mwanamke mwenye hedhi.”

Kwa hiyo watu wa Jeddah na watu wa Twaa-if si miongoni mwa wakazi wa Makkah, si miongoni mwa watu wa Haram. Ikiwa watataka kuondoka baada ya Hajj, basi ni juu yao kufanya Twawaaf-ul-Wadaa´. Ama kuhusu ´Umrah, jambo lake ni pana na rahisi zaidi. Wakifanya Twawaaf-ul-Wadaa´ ndio bora zaidi. Wakiacha, basi yaliyo sahihi ni kwamba si lazima kuaga katika ´Umrah. Hata hivyo ni lazima katika Hajj kwa mujibu wa maoni sahihi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30132/هل-على-اهل-جدة-طواف-وداع-وما-الدليل
  • Imechapishwa: 12/09/2025