Twawaaf-ul-Wadaa´ kwa anayefanya ´Umrah

Swali: Vipi kuhusu Twawaaf-ul-Wadaa´ kwa mwenye kufanya ´Umrah?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba Twawaaf-ul-Wadaa´ kwa mwenye kufanya ´Umrah ni wajibu. Isipokuwa ikiwa mtu anarudi kutoka safari yake papohapo kwa njia ya kwamba ametufu, akafanya Sa´y, akapunguza kisha akapanda gari yake na kurudi. Huyu itamtosha ile Twawaaf ya kwanza. Ama akibaki, japo saa moja tu, basi ni lazima kwake kufanya Twawaaf-ul-Wadaa´ wakati wa kutoka.

Check Also

Twawaaf-ul-Wadaa´ baada ya ´Umrah

Swali: Mtu ambaye amefanya ´Umrah ni lazima afanye Twawaaf-ul-Wadaa´? Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa …