Twahara ya mwenye damu ya ugonjwa na anayesumbuliwa na mkojo wa mara kwa mara

Swali: Je, mtu mwenye damu ya ugonjwa na mwenye ugonjwa wa kutokwa na  mkojo hovyo wanatakiwa kutawadha juu ya kila swalah?

Jibu: Ndio, wanatakiwa kutawadha kila wakati, sio kwa ajili ya kila swalah, bali kwa kila wakati.

Swali: Unakusudia kila faradhi?

Jibu: Ikiwa ataoga au kutawadha kwa ajili ya Dhuhr, basi itafaa kuswali wakati wa adhuhuri zile swalah anazotaka, asome Qur-aan na kutufu Ka´bah ya Makkah mpaka wakati wa alasiri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24757/هل-يتطهر-صاحب-السلس-والمستحاضة-لكل-وقت
  • Imechapishwa: 07/12/2024