Yahyaa bin Yahyaa at-Taymiy, Ja´far bin ´Abdillaah na kundi la wengine wamesema:
“Kuna mtu alikuja kwa Maalik bin Anas akasema: “Ee Abu ´Abdillaah:
الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ
“Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]
“Yuko juu namna gani?”
Sijawahi kumuona Maalik anachukulia vibaya kama alivofanya siku hiyo. Akaanza kutokwa na jasho na wasikilizaji wakasubiri wamsikie atasema nini. Kisha akasema:
“Namna haifahamiki. Kuwa Kwake juu si kwamba hakufahamiki. Ni wajibu kuliamini hilo na kuuliza juu yake ni Bid´ah. Mimi nachelea wewe ni mpotevu.”
Kisha akaamrisha atolewe nje.
Haya yamethibiti kutoka kwa Maalik. Hii ndio ´Aqiydah ya Salaf. Hatufahamu namna Alivyo juu, ni kitu hatukijui kabisa. Kuwa Kwake juu kunajulikana, kama alivyotujuza katika Kitabu Chake, na ni kwa njia inayolinagana Naye. Hatuingii kwa undani katika jambo hilo na hatuleti uchambuzi, hatuingii katika malazimisho yanayopelekea katika hilo, si kwa kukanusha wala kwa kuthibitisha. Bali tunanyamaza na tunasimama pale waliposimama Salaf. Tutambue kuwa lau Kuwa juu kungelifasiriwa basi Maswahabah na Taabi´uun wangelikuwa wa mwanzo kufanya hivo. Midhali waliweza kukubali, wakalipitisha na kulinyamazia, tukajua kwa yakini kabisa kwamba Allaah (Jalla Jalaaluh) hawezi kufananishwa na yeyote katika sifa Zake, kustawa Kwake na kushuka Kwake. Ametakasika na kasoro na mapungufu kutokamana na yale wanayosema madhalimu.
[1] 20:05
- Muhusika: Imam Shams-ud-Dîn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 141-142
- Imechapishwa: 20/02/2019
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
08. Ee Maalik, amelingana vipi juu ya ´Arshi?
Abul-Hasan ´Abdur-Rahmaan bin Ibraahiym bin Muhammad bin Yahyaa al-Muzakkiy ametukhabarisha: Muhammad bin Daawuud bin Sulaymaan amenihadithia: ´Aliy bin Muhammad bin ´Ubayd Abul-Hasan amenikhabarisha: Abu Yahyaa bin Bishr al-Warraaq ametuhadithia: Muhammad bin al-Ashras al-Warraaq Abu Kinaanah ametuhadithia: Abul-Mughiyrah al-Hanafiy ametuhadithia: Qurrah bin Khaalid ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa mama yake,…
In "´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth"
Kanuni ya Maalik inatumika katika sifa zote
Wakati kuliposemwa kuambiwa Maalik bin Anas (Rahimahu Allaah): ”Ee Abu ´Abdillaah! الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ “Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1] Amelingana vipi?” Maalik akaanza kutokwa na jasho na wasikilizaji wakasubiri wamsikie atasema nini. Akainua kichwa chake kisha akasema: ”Kulingana si kwamba ni jambo lisilofahamika na namna haitambuliki. Ni…
In "Salaf na Tafwiydhw"
39. Maneno ya Imaam Maalik kuhusu kulingana kwa Allaah
Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema: Imaam Maalik bin Anas (Rahimahu Allaah) aliulizwa: “Ee Abu ´Abdillaah! الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ ”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1] Amelingana namna gani?” Akajibu: “Kulingana kunajulikana na namna haijulikani. Kuamini hilo ni wajibu na kuulizia hilo ni Bid´ah.” Kisha akaamrisha mtu yule atolewe…
In "Sharh Lum´at-il-I´tiqaad - Ibn ´Uthaymiyn"