Swali: Shaytwaan na marafiki wabaya wanawatatiza baadhi ya vijana katika suala la makadirio na kwamba hakuna faida ya kushikamana na dini muda wa kuwa jambo hilo tayari limekwishaamuliwa. Tunatarajia maelekezo kutoka kwenu?
Jibu: Shubuha hii ilikwishatokea zamani katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Iliwatokea kwa Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowahadithia na kusema:
”Hakuna yeyote kati yenu isipokuwa amekwishajulikana makazi yake ya Peponi na makazi yake ya Motoni.” Wakasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Basi ni ya nini matendo wakati huo?” Akasema: ”Fanyeni matendo, kwani kila mtu atarahisishiwa kwa lile aliloumbiwa. Ama watu wa furaha watarahisishiwa kwa matendo ya watu wa furaha, na ama watu wenye kula khasara watarahisishiwa kwa matendo ya watu wenye kula khasara.” Kisha akasoma maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
فَأَمَّا مَنْ أَعْطَىٰ وَاتَّقَىٰ وَصَدَّقَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْيُسْرَىٰ وَأَمَّا مَن بَخِلَ وَاسْتَغْنَىٰ وَكَذَّبَ بِالْحُسْنَىٰ فَسَنُيَسِّرُهُ لِلْعُسْرَىٰ
“Basi yule anayetoa na akamcha Allaah na akasadikisha lililo jema zaidi, basi tutamuwepesishia kwa yaliyo mepesi. Ama yule afanyaye ubakhili na akajiona amejitosheleza na akakadhibisha lililo jema zaidi, basi tutamuwepesishia kwa yaliyo magumu.”[1][2]
Hii inatufafanulia kuwa makadirio tayari yamekwishaamuliwa, kwamba Allaah amekwishajua kila kitu na kukidhibiti kila kitu. Lakini ameweka kwa hili sababu na kwa lile sababu. Kwa mema zipo sababu na kwa maovu zipo sababu. Pepo ina matendo yake na Moto yana matendo yake. Kwa hiyo yule mwenye kuwa katika watu wa furaha basi Allaah atampa tawfiyq ya matendo ya watu wa furaha na vilevile atamsaidia. Na mwenye kuwa katika watu wa wenye kula khasara atarahisishiwa kwa matendo ya watu wa wenye kula khasara.
Kwa hiyo ni juu ya muumini ajitahidi katika matendo anayoyajua kuwa ni mazuri na kwamba ni katika matendo ya watu wa furaha. Ni juu ya muumini ajitahidi jambo hilo, afanye haraka kuyatekeleza na ayazidishe. Sambamba na hayo ajihadhari na matendo ambayo Allaah ameyafanya kuwa miongoni mwa matendo ya watu wenye kula khasara, ayaepuke na ayaweke mbali na awatishie watu nayo.
[1] 92:05-10 al-Bukhaariy (4949) na Muslim (2647).
[2] al-Bukhaariy (1362) na Muslim (2647).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29988/ما-الرد-على-شبهة-ترك-العمل-لان-القدر-فرغ-منه
- Imechapishwa: 25/08/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29988/ما-الرد-على-شبهة-ترك-العمل-لان-القدر-فرغ-منه
Imechapishwa: 25/08/2025
https://firqatunnajia.com/tuache-matendo-kwa-sababu-kila-kitu-kimeshaamuliwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket