Tovuti zinazofundisha kutumia majini

Swali: Kuna tovuti ambazo mtu anaweza kujifunza namna ya kulileta jini na kulitumikisha. Je, inajuzu kwa mtu kuziingia kwa ajili tu ya kujua kilichomo ndani?

Jibu: Hapana. Hatakiwi wala kuzitazama. Ajitenge nazo mbali. Ni majanga yaliyotokea leo kwenye masimu na kwenye njia za mawasiliano. Kunaenezwa kupitia njia hizo shari na kunalinganiwa katika batili. Muislamu anatakiwa kujitenga nazo mbali. Simu zinatumiwa kwa ajili ya haja, pindi unapotaka kumzungumzisha mtu au pindi mtu anapotaka kukuzungumzisha. Mbali na haya usidanganyike na yale yenye kuenezwa ndani yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (36) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majd%20-%2030%20-%2012%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 30/09/2020