Tofauti ya uadilifu na udhibiti wa mpokezi

Swali: Ikiwa wanazuoni wamezungumza kuhusu dini ya mpokezi, lakini hawakuzungumza kuhusu hifdhi na usahihi wake?

Jibu: Hilo linahusiana na uadilifu, kwani uadilifu ni kitu kimoja, na usahihi na udhibiti ni kitu kingine.

Huenda mtu akawa ni mwadilifu lakini si mwenye udhibiti. Kwa maana nyingine ana udhaifu wa kuhifadhi.

Huenda akawa ni mwenye udhibiti mzuri upande wa hifdhi, lakini si mwadilifu. Kwa maana nyingine ana ufuska, maasi au Bid´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31308/ما-الفرق-بين-العدالة-والضبط-في-رواة-الحديث
  • Imechapishwa: 18/10/2025