Mpokezi anayefanya hadaa mwaminifu

Swali: Vipi mpokezi mwenye kufanya hadaa (التدليس) anayesimulia kwa mtindo wa kutotaja namna ya upokeaji (عنعنة) ikiwa kumekuwepo kukutana naye na ni mwenye kuaminika?

Jibu: Haisaidii kitu. Ikiwa hakuwa wa wakati mmoja naye, basi haihesabiki kuwa amesikia, tofauti na yule ambaye aliishi wakati wake katika mfano wa kijiji chake, mji wake au sehemu yake. Ama yule ambaye hakuwahi kuishi wakati wake, bali alizaliwa baada yake, basi hiyo ni cheni ya wapokezi iliyokatika.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31303/ما-حكم-عنعنة-المدلس-الثقة-في-الحديث
  • Imechapishwa: 18/10/2025