Tofauti ya msikiti na mahali pa kuswalia

Swali: Kuna tofauti gani kati ya msikiti na sehemu ya kuswalia (مصلى)?

Jibu: Kutokana na utambulisho wa ujumla, kila ardhi ni msikiti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ardhi nzima imefanywa kwangu mimi na ummah wangu kuwa ni mahali pa kuswalia na yenye kusafisha.”[1]

Kuhusu utambulisho maalum, msikiti ni mahali kulipoandaliwa kwa ajili ya kuswalia maeneo hayo. Ni mahali maalum kwa ajili ya kuswalia, ni mamoja umejengwa kwa mawe, udongo, simenti au haukujengwa kabisa.

Kuhusu mahali pa kuswalia ni pale pahali ambapo mtu anaswalia lakini sio daima. Anaswalia maeneo hapo wakati kunapoingia wakati wa swalah na mahali hapo hapawi ni msikiti. Dalili ya hilo ni kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali nyumbani kwake swalah za kujitolea, lakini nyumba yake haikuwa ni msikiti. Vivyo hivyo ´Utbaan bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) alimwita Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nyumbani kwake apaswalia ili baadaye maeneo hayo ´Utbaan apafanye kuwa ni mahali pa kuswalia, lakini maeneo hayo ´Utbaan hakupafanya kuwa ni msikiti. Kwa hivyo mahali pa kuswalia ni maeneo ambayo kumeandaliwa kwa ajili ya kuswalia pasi na kulengeshwa kuwa ni msikiti.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/394-395)
  • Imechapishwa: 23/04/2026