Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa saa iliyopambwa kwa dhahabu?
Jibu: Ni jambo linalotambulika kwamba dhahabu ni haramu kwa wanaume. Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwona bwana mmoja mkononi mwake amevaa pete ya dhahabu, akaichukua na kuitupa na akasema: “Je, hivi kweli mmoja wenu anakusudia kuweka kaa la moto mkononi mwake?”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Dhahabu na fedha vimehalalishwa kwa wake wa ummah wangu na vimeharamishwa kwa waume wa ummah wangu.”[2]
Kwa hivyo haijuzu kwa wanaume kuvaa kitu chochote kilicho na dhahabu, ni mamoja pete, zipu au kitu kingine kukiwemo saa ikiwa iko na dhahabu.
Lakini ikiwa saa imepambwa tu kwa dhahabu au ikawa muonekano wake tu ndio wa dhahabu au ikawa iko na vinukta vidogo vya dhahabu, ni jambo linalofaa ingawa hatupendekezi kwa wanaume kuvaa saa kama hizo. Kwa sababu watu hawatambui kuwa imepambwa tu dhahabu au kwamba ni dhahabu iliyochanganywa na nyenzo za saa hii. Watu wataanza kumdhania vibaya mtu huyu. Kuna khatari wakaanza kumwigiliza ikiwa ni miongoni mwa wale watu wanaogilizwa na matokeo yake wakaanza kuvaa dhahabu tupu au saa zilizochanganywa na dhahabu. Kwa hivyo siwapendekezi wanaume kuvaa saa zilizopambwa kwa dhahabu, ingawa ni halali. Yale ambayo ni halali yanatosheleza na ni mengi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yeyote mwenye kujiepusha na shubuha basi ameitakasa dini na heshima yake.”[3]
Lakini ikiwa upambwaji ni wa dhahabu na nyenzo nyenginezo, basi kuna uwezekano mkubwa ikawa ni haramu.
[1] Muslim (2090).
[2] Ahmad (1/96) na (1/115), Abu Daawuud (4057) na an-Nasaa’iy (3595). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Aadaab-uz-Zifaaf”.
[3] al-Bukhaariy (52) na Muslim (1599).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/360-361)
- Imechapishwa: 23/04/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/360-361)
Imechapishwa: 23/04/2026
https://firqatunnajia.com/saa-zilizopambwa-kwa-dhahabu/