Ama kuhusu Sunnah, Hadiyth Swahiyh zilizopokelewa na kikosi cha Maswahabah zinasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha kupangusa, katika baadhi yake akatoa ruhusa ya kupangusa na katika nyingine alifanya kufuta kwa mkazi mchana mmoja na usiku wake na kwa msafiri michana mitatu na nyusiku zake. Ni wazi sana kwamba Hadiyth ni kama maandishi yaliyo wazi juu ya kuanza muda wa kufuta tangu upangusaji wa kwanza. Pia ni kama maandishi yaliyo wazi juu ya kurudisha maoni ya kwanza, kwa sababu maana yake – kama walivyosema katika matawi ya Fiqh – ni kwamba mwenye kuswali Fajr karibu na kuchomoza jua, kisha akapata hadathi wakati wa Fajr ya siku ya pili, kisha akatawadha na kufuta mara ya kwanza kwa ajili ya swalah ya Fajr, basi hana kufuta baada yake. Je, anazingatiwa mtu kama huyu kwamba amepangusa mchana mmoja na usiku wake? Kwa mujibu wa maoni ya pili na yenye nguvu ni kwamba inafaa kwake kupangusa mpaka karibu na Fajr ya siku ya tatu.
Bali wamesema jambo la ajabu zaidi kuliko tulilotaja: lau akipata hadathi na akapangusa baada ya kupita mchana mmoja na usiku wake au michana mitatu na nyusiku zake, kutegemea kama ni mkazi au msafiri, basi muda wa kupangusa umemalizika na haijuzu kupangusa baada ya hapo. Badala yake anapaswa kuzivaa upya akiwa katika hali ya twahara. Kwa msemo mwingine wakamnyima kunufaika na ruhusa hii kwa kujengea juu ya maoni haya yanayopingana na Sunnah. Kwa sababu hiyo Imaam an-Nawawiy, ambaye kawaida hujitahidi kutoenda kinyume na madhehebu yake, hakuona jengine isipokuwa kwenda kinyume na madhehebu yake kutokana na nguvu ya dalili katika suala hili.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Itmaam-un-Nush fiy Ahkaam-il-Mash, uk. 89-90
- Imechapishwa: 23/04/2026
Ama kuhusu Sunnah, Hadiyth Swahiyh zilizopokelewa na kikosi cha Maswahabah zinasema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliamrisha kupangusa, katika baadhi yake akatoa ruhusa ya kupangusa na katika nyingine alifanya kufuta kwa mkazi mchana mmoja na usiku wake na kwa msafiri michana mitatu na nyusiku zake. Ni wazi sana kwamba Hadiyth ni kama maandishi yaliyo wazi juu ya kuanza muda wa kufuta tangu upangusaji wa kwanza. Pia ni kama maandishi yaliyo wazi juu ya kurudisha maoni ya kwanza, kwa sababu maana yake – kama walivyosema katika matawi ya Fiqh – ni kwamba mwenye kuswali Fajr karibu na kuchomoza jua, kisha akapata hadathi wakati wa Fajr ya siku ya pili, kisha akatawadha na kufuta mara ya kwanza kwa ajili ya swalah ya Fajr, basi hana kufuta baada yake. Je, anazingatiwa mtu kama huyu kwamba amepangusa mchana mmoja na usiku wake? Kwa mujibu wa maoni ya pili na yenye nguvu ni kwamba inafaa kwake kupangusa mpaka karibu na Fajr ya siku ya tatu.
Bali wamesema jambo la ajabu zaidi kuliko tulilotaja: lau akipata hadathi na akapangusa baada ya kupita mchana mmoja na usiku wake au michana mitatu na nyusiku zake, kutegemea kama ni mkazi au msafiri, basi muda wa kupangusa umemalizika na haijuzu kupangusa baada ya hapo. Badala yake anapaswa kuzivaa upya akiwa katika hali ya twahara. Kwa msemo mwingine wakamnyima kunufaika na ruhusa hii kwa kujengea juu ya maoni haya yanayopingana na Sunnah. Kwa sababu hiyo Imaam an-Nawawiy, ambaye kawaida hujitahidi kutoenda kinyume na madhehebu yake, hakuona jengine isipokuwa kwenda kinyume na madhehebu yake kutokana na nguvu ya dalili katika suala hili.
Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Itmaam-un-Nush fiy Ahkaam-il-Mash, uk. 89-90
Imechapishwa: 23/04/2026
https://firqatunnajia.com/07-mfano-wa-kwanza-wa-muda-wa-kupangusa-juu-ya-soksi/