Wanazuoni katika suala hili wana mitazamo miwili mashuhuri:

1 – Unaanza tangu wakati wa kupatwa na hadathi baada ya kuzivaa.

2 – Unaaza tangu kufuta baada ya kupatwa na hadathi.

Abu Haniyfah, ash-Shaafi´iy, Ahmad na wafuasi wao wameonelea maoni ya kwanza. Hatujui kuwa na dalili inayostahiki kutajwa isipokuwa maoni tu. Kwa sababu hiyo baadhi ya wafuasi wao wameenda kinyume nao, kama itakavyokuja baadaye. Sijui kuwa kuna yeyote miongoni mwa Maswahabah ambaye alionelea mtazamo wao, kinyume na wafuasi wa mtazamo wa pili; wanaongozwa na Hadiyth Swahiyh na fatwa ya ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-un-Nush fiy Ahkaam-il-Mash, uk. 88-89
  • Imechapishwa: 23/04/2026