05. Wudhuu´ wa ambaye alipangusa juu ya soksi kisha akazivua

Kuhusu yale yaliyopokelewa na Ibn Abiy Shaybah (1/187) na al-Bayhaqiy (1/289) kutoka kwa mtu miongoni mwa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye aliulizwa kuhusu mtu anayepangusa juu ya soksi zake kisha akazivua. Akajibu:

”Aoshe miguu yake.”[1]

Katika cheni ya wapokezi wake yumo Yaziyd bin ´Abdir-Rahmaan ad-Daalaaniy. Haafidhw Ibn Hajar amesema juu yake:

”Ni mkweli, lakini anakosea sana na alikuwa anafanya hadaa.”

al-Bayhaqiy amepokea mfano wa hayo kutoka kwa Abu Bakrah. Wapokezi wake ni wenye kuaminika isipokuwa ´Aliy bin Muhammad al-Qurashiy, sikumjua.

Kisha akaipokea kutoka kwa al-Mughiyrah bin Shu´bah, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Kufuta juu ya soksi za ngozi ni michana mitatu na nyusiku zake kwa msafiri, na mchana mmoja na usiku wake kwa mkazi maadamu hajazivua.”

Kisha akasema tena:

”´Umar bin Rudayh ameisimulia peke yake. Na si mwenye nguvu.”

Ziada hii ”maadamu hajazivua” ni nyonge na inayopingana kwa sababu ya mpokezi huyu dhaifu kuisimulia peke yake na pia kwa kukosekana nyingine yenye kuitia nguvu.

[1] Ibn Abiy Shaybah (1/187) na al-Bayhaqiy (1/289).

  • Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-un-Nush fiy Ahkaam-il-Mash, uk. 88
  • Imechapishwa: 23/04/2026