Tofauti ya Ahl-us-Sunnah na Ahnaaf katika imani ni ya kimatamshi tu?

Swali: Shaykh-ul-Islaam amesema kwamba tofauti kati yetu na Ahnaaf ni ya kimatamshi?

Jibu: Sikuwahi kuyaona kwa Shaykh-ul-Islaam. Nadhani hayo yametajwa na Ibn Abiyl-´Izz, ama kutoka kwake mwenyewe au kutoka kwa mwingine. Hata hivyo si sahihi. Siyo ya kimatamshi, bali ni ya kweli. Wakisema kuwa mtu anastahiki kuingia Peponi akiwa na imani kamili, hiyo ni tofauti ya kweli na si ya kimatamshi tu. Lakini wakisema kuwa mtu sampuli hiyo hastahiki Peponi, kwamba yuko chini ya utashi wa Allaah, kwamba imani yake si kamili na kwamba yuko katika hali ya khatari, hiyo ndio inazingatiwa kuwa ni tofauti ya kimatamshi. Lakini ni kosa wakisema kuwa [matendo] si katika imani na kwamba ni yenye kukamilisha tu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31046/هل-الخلاف-بين-اهل-السنة-والاحناف-في-الايمان-لفظي
  • Imechapishwa: 26/09/2025