Tofauti kati ya watu hawa wawili wenye kukhalifu Sunnah

Bid´ah ni ile ambayo mtu amelazimiana nayo, sawa katika matendo, maneno au mambo ya imani. Si sawa kusema kwamba mwenye kukosea mara moja katika mambo ya imani na akawa hakulazimiana na hilo ya kwamba ni mtu wa Bid´ah. Vililevile na kwa yule mwenye kufanya kitendo kinachoenda kinyume na Sunnah ya kwamba ni mtu wa Bid´ah lau atafanya mara moja, mara mbili n.k. na akawa hakulazimiana na hilo. Kulazimiana nayo ni kidhibiti muhimu, kama alivyosema Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah katika baadhi ya maneno yake ya kwamba kidhibiti cha kulazimiana ni muhimu katika kutofautisha kati ya Bid´ah na kwenda kinyume na Sunnah. Katika hali hii tunasema kuwa mtu huyu ameenda kinyume na Sunnah katika kitendo chake na hatusemi kuwa ni mtu wa Bid´ah isipokuwa pale ambapo atalazimiana na kwenda kwake kinyume na Sunnah na hilo akalifanya kuwa ni Dini. Kwa hivyo, mwenye kukosea katika kitendo miongoni mwa matendo ya ´ibaadah na akaenda kinyume na Sunnah katika kitendo hicho, ikiwa anajikurubisha kwa Allaah kwa kitendo hicho tunasema kuwa kitendo chako hichi kinaenda kinyume na Sunnah. Akiendelea kulazimiana na kitendo hicho siku zote baada ya ubainifu, hapo ndipo atafanyiwa Tabdiy´. Hichi ni kidhibiti muhimu katika kutofautisha kati ya Bid´ah na kwenda kinyume na Sunnah.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah (05)
  • Imechapishwa: 17/05/2020