Thawabu za anayemfanyia Hajj au ´Umrah mwengine

Swali: Je, mtu analipwa thawabu akimfanyia hajj au ´umrah mtu mwengine?

Jibu: Ndio. Analipwa thawabu kwa kule kuswali ndani ya msikiti Mtakatifu, kusimama sehemu za ´ibaadah na za du´aa. Thawabu za ´ibaadah za hajj zinamwendea yule mtu alimuhijia anayemuwakilisha na ziada ya kheri zote zinaenda kwa yule muwakilishaji.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (20) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-6-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 29/12/2019