Thawabu kwa anayeoa wake wengi kwa ajili ya kukithirisha kizazi?

Swali: Anayeoa msichana bikira kwa ajili ya kufanyia kazi Sunnah na hahitaji jambo hilo?

Jibu: Akiwa na uwezo aoe wanne.

Swali: Anaoa kwa ajili ya kupata thawabu?

Jibu: Allaah amjaze kheri. Allaah amfanye imara yeye na sisi.

Swali: Kuhusiana na watoto mtu anaweza kusema kuwa inapendeza kuoa mwanamke mwengine kwa ajili ya kupata watoto wengi?

Jibu: Udhahiri ni kwamba inatakikana, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Oeni wanawake wenye kuzaa sana na wenye mahaba, kwani hakika mimi nitajifakhari kwa ajili yenu siku ya Qiyaamah.”[1]

Akioa kwa ajili ya nia hii ni jambo zuri kwa ajili ya kupata watoto wengi. Katika hali hiyo aoe mke wa tatu na wa nne. Akiwa na uwezo bila ya uzito hapana vibaya. Ni jambo zuri.

[1] Ahmad na at-Twabaraaniy kwa mlolongo wa wapokezi mzuri Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23902/حكم-من-يعدد-لاجل-السنة-وتحصيل-الولد
  • Imechapishwa: 30/05/2024